Imeandikwa na Issa Mnally na Dustan Shekidele, Morogoro
AMA kweli dunia imefika ukingoni! Ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, bado ipo kazini ikishirikiana na polisi ambapo safari hii imeibuka na kigongo cha aina yake baada ya kumnasa ‘mwanaume tata’ akijihusisha na ukahaba, Risasi Mchanganyiko lina mzigo kamili.
AMA kweli dunia imefika ukingoni! Ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, bado ipo kazini ikishirikiana na polisi ambapo safari hii imeibuka na kigongo cha aina yake baada ya kumnasa ‘mwanaume tata’ akijihusisha na ukahaba, Risasi Mchanganyiko lina mzigo kamili.
Ikiwa kwenye fumuafumua ya magenge ya ngono maeneo ya Kahumba mjini Morogoro hivi karibuni, OFM kwa mwaliko wa jeshi la polisi, ilipigwa na butwaa baada ya kukutana uso kwa uso na mwanaume huyo aliyekuwa amejumuika katikati ya kundi la madadapoa naye akifanya kama wao.
Mbali na jamaa huyo ambaye jina lake halikupatikana, baadaye ilibainika kuwa kulikuwa na wenzake wawili ambao ilikuwa vigumu kuwatambua kufuatia kujiremba kupita hata wanawake wenyewe.
Kuna madai kwamba kijana huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 20 - 24 ni mtoto wa kigogo serikalini na amekuwa akijichanganya na madadapoa hao kwa muda mrefu.
Mara baada ya kunaswa, kijana huyo aliangua kilio huku akidai kuumbuka kwani familia yake wakiiona picha yake hawatamwelewa.
“Naombeni tumalizane hapahapa kwani nyumbani hawafahamu kuwa nipo hapa muda huu. Hii ni kesi kubwa kwangu nisaidieni,” alisikika kijana huyo.
Hata hivyo, pamoja na kilio hicho, polisi hawakumwelewa, alibebwa juujuu na kuingizwa katika karandinga kisha kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Wakazi wa maeneo hayo walikuwa wakilalamika mara kwa mara kutokana na kurundikana kwa makahaba mahali hapo na kusababisha uchafuzi wa mazingira kwa kutupa ovyo mipira ya kiume (kondom).
Katika msako huo, wanaume hao watatu walijumuishwa na wanawake 20 waliokamatwa wakijihusisha na biashara haramu ya kuuza miili.
0 comments:
Post a Comment