Imelda Mtema na Musa Mateja
STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amedhihirisha kuwa ni sikio la kufa baada ya kusema yeye ni miongoni mwa wanawake wanaojua kuchuna mabuzi.
Kauli hiyo imechochea vigezo vya kumfanya Shilole aonekane hasikii kwani wiki kadhaa zilizopita mchungaji wa kanisa moja lililopo Ubungo, jijini Dar ambaye hakujulikana jina lake, alimtaka kuishi katika sura ya kumpendeza Mungu lakini inaonekana amempuuza.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, jijini Dar es Salaam, Shilole alisema alitunga wimbo wa Nachuna Buzi kwa sababu anajua kuwa wanawake wengi ni mafundi wa tabia hiyo akiwemo yeye mwenyewe!
“Unajua mwanamuziki unatakiwa kuchagua wimbo ambao unaigusa jamii nzima kwani mambo ya kuchuna mabuzi kwa wanawake yapo sana, hata mimi mwenyewe ni mtaalamu wa kuchuna mabuzi,” alisema Shilole.
Hata hivyo alisema japokuwa ana tabia hiyo lakini anatambua siyo nzuri hivyo anawasihi wanawake wengine kuachana nayo kwani ipo siku itawaingiza matatizoni.
Mbali na mchungaji huyo, juzi Jumapili, Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Ukonga –Mazizini, Dar, Emmanuel Kapande alimtumia ujumbe wa watoto wa Shule ya Jumapili (Sunday School) nyumbani kwake kwa lengo la kuimba na kufanya maombi.
Watoto hao walifika nyumbani kwa Shilole, Mwananyamala - Manjunju, wakiwa wameongozana na walimu wao, Jonas Timotheo, Rehema Ezra na Catherine Libogoma.
Ujumbe huo, ulimpelekea baraka ya maombi nyumbani kwake na kumshauri aishi katika mazingira yanayompendeza Mungu.
0 comments:
Post a Comment