Sunday, February 9, 2014


Mtoto wa marehemu Dk. Mgimwa, Godfrey Mgimwa atakayegombea Jimbo la Kalenga CCM.
MATOKEO ya  kura  za maoni  ndani ya  CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo huku mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa  Jimbo hilo, Godfrey Mgimwa akishinda kwa  kishindo  katika  nafasi hiyo, akifuatiwa na Jackson Kiswaga katika matokeo hayo.
Godfrey Mgimwa amepata  kura 342 huku Kiswaga akipata kura 170 na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Hafsa Mtasiwa akiambulia  kura 42 .
Matokeo hayo  yaliyotangazwa katika ukumbi wa Shule ya  Sekondari  Mwembetogwa mjini Iringa yanaonesha mgombea Peter Mtisi kapata kura 33, Msafiri Pangagira kura 8, Bryson Kibasa kura 7, Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2.
Chanzo: Matukiodaima.com

0 comments:

Post a Comment