Friday, February 7, 2014


Washitakiwa wakipelekwa kizimbani.
Msafara wa kuelekea kizimbani.
Wakisubiri kupandishwa kizimbani.
Mmoja wa washitakiwa akionesha ishara ya vidole viwili.
Wakiwa kizimbani baada ya kutajiwa shitaka lao.
RAIA 11 wa Iran, leo wamepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar wakikabiliwa na shitaka la kunaswa na shehena ya madawa ya kulevya wakiwa kwenye meli. Washitakiwa hao walisomewa mashitaka yao na Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo, Hellen Moshi, mbele Hakimu wa mahakama hiyo, Nyigulila Mwaseba ambapo hawakutakiwa kujibu chochote mpaka Februari 24 kesi hiyo itakapotajwa tena.
PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL

0 comments:

Post a Comment