WANAWAKE WAWILI WALIUAWA NA WAUME ZAO KATIKA MATUKIO MAWILI WILAYANI CHUNYA. KATIKA TUKIO LA KWANZA LILILOTOKEA MNAMO TAREHE 06.02.2014 MAJIRA YA SAA 07:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGNES DAUD (32) MKAZI WA KIJIJI CHA SHOGA ALIKUTWA AMEUAWA NA MUME WAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THOMAS @MSUKUMA KWA KUMKATA KOROMEO KWA KUTUMIA KISU. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KATIKA KIBANDA WALICHOKUWA WANAISHI NA MUME WAKE KATIKA KAMBI YA UCHIMBAJI MADINI MALI YA ISACK MAMBO. KATIKA TUKIO LA PILI LILILOTOKEA SIKU HIYO HIYO MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONIHUKO KATIKA KITONGOJI CHA LONDON WILAYANI CHUNYA MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEFROZA GIDION (18) MKAZI WA KIJIJI CHA ISANZU ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MUME WAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA JANUARI. TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI MAREHEMU AKIWA NYUMBANI. VYANZO VYA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI. WATUHUMIWA WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA MATUKIO HAYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.
MWENDESHA BODABODA AFARIKI
DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
MNAMO TAREHE 07.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI HUKO KATIKA ENEO LA KILIMO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.893 BPD AINA YA ISUZU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EMANUEL NSOLO (31) MKAZI WA KIKONDO LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.322 CTJ AINA YA SHINERAY AITWAYE OSWARD NDUNGURU (26) MKAZI WA IGANZO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE AITWAYE GETRUDA CHARLES MWAKALOBO (28) MKAZI WA IGANZO. MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI DEREVA WA GARI KUKATISHA BARABARA BILA KUCHUKUA TAHADHARI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WATU WAWILI WAKAMATWA WAKIWA
NA NOTI BANDIA MKOANI MBEYA.
NA NOTI BANDIA MKOANI MBEYA.
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA PATRICK MSIGWA (34)NA ANTHONY MWAKIFWAMBA (32) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISYONJE WALIKAMATWA NA WANANCHI WAKIWA NA NOTI BANDIA 57 @ TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS 285,000/=. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 07.02.2014 MAJIRA YA SAA 15:30HRS ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SIMAMBWE WILAYA YA MBEYA VIJIJNI BAADA YA WATUHUMIWA HAO KUKAMATWA NA WANANCHI WAKATI WAKIWA WANANUNUA CHIPS NA KUTOA NOTI MOJA YA TSHS 5,000/= NA WALIPOBANWA NDIPO WALIPOONYESHA NOTI NYINGINE. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI WANAPO POKEA/TUMIA NOTI ILI KUEPUKA KUTAPELIWA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment