Friday, February 7, 2014


Na Waandishi Wetu
SHABASHIII! Arobaini (40) za mke wa mtu zimetimia baada ya kunaswa ndani ya gari akifanya uzinifu na kijana mmoja mtanashati ‘Sharobaro’ aliyejitambulisha kwa jina la Athumani (26) maeneo ya Bamaga Mwenge, jijini Dar.
Sharobaro baada ya kufumwa na mke wa mtu.
Tukio hilo lilitokea usiku wa manane Februari 4, baada ya mke  huyo aliyetambulika kwa  jina moja la Husna na sharobaro wake kujiingiza kwenye mtego wa OFM na kunasa wazimawazima.
Awali, OFM ilipata malalamiko kutoka kwa majirani zake kwamba pamoja na kufanya kazi nzuri ndani na nje ya Dar lakini imeyasahau maeneo ya karibu na makao yake makuu, hivyo kutakiwa kuyafanyia kazi haraka.
Sharo akiwa na aibu baada ya kunaswa akijivinjari na mke wa mtu kwenye gari bovu.
“Jamani  OFM si mnafanya kazi kila siku hapa Dar na mikoani kiasi cha kujizolea sifa kemkemu? Sasa mbona hapa maeneo ya Bamaga mnapasahau? Tunapata tabu wakazi wa hapa, wanawake wanaojiuza wanafanya mapenzi kila kona hatuna raha,” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Gari bovu walimokutwa wawili hao.
Baada ya kupata taarifa hizo na kuzifanyia uchunguzi yakinifu, OFM ilijipanga na kuweka mtego wake.
Mtego huo uliwekwa maeneo yote yanayodaiwa kutisha kwa vitendo hivyo huku ikitoa taarifa Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’.
Ilipotimia saa 7 usiku makamanda wa OFM waliokuwa kazini walimshuhudia mteja mmoja akimnunua changudoa na kuingia naye ndani ya gari moja bovu lililopo maeneo ya Bamaga karibu na kituo cha daladala kisha wakajifungia.
Mke wa mtu baada ya kunaswa na sharo.
Haraka makamanda wa kikosi hicho waliwasiliana na polisi na kuwapa dakika chache wazinzi hao ili waanze kufanya yao, baada ya muda huo kutimia,  OFM waliwavamia na kuwanasa.
Mara baada ya kunaswa na kutakiwa kuvaa nguo zao, Sharobaro aliomba asipelekwe polisi na kuapa kutorudia tena huku akimtupia lawama zote mwanamke aliyekuwa naye na kudai  kwamba tangu mwanzo alikuwa na wasiwasi juu ya ‘kufurahishana’ karibu na makao makuu ya ofisi za OFM.
Baadhi ya kondom zilizotumika zikiwa eneo hilo.
“Jamani naomba msinipeleka kituoni, sitarudia tena kufanya mapenzi maeneo haya. Mkamateni huyu mwanamke ambaye ndiye aliyenileta hapa wakati tangu mwanzo moyo wangu ulikuwa unasita,” alisema.
Naye mwanamke huyo alisema kuwa kukamatwa kwake ni kama ajali kazini kwa kuwa tangu aanze biashara hiyo amekamatwa mara nyingi lakini si katika mazingira kama hayo.
Mke wa mtu akitolewa kwenye gari bovu baada ya kunaswa akiwa na sharo.
“Jamani nimekamatwa mara nyingi sana lakini siyo katika mazingira ya aibu kama haya, hata mwenyewe sijapenda,” alisema mwanamke huyo.
Hatimaye wote wawili walichukuliwa na polisi na kupelekwa kituoni na  kufunguliwa jalada la kesi KJM/RB/ 1081/2014.
Hata hivyo, taarifa tulizozipata wakati tukienda mitamboni kutoka kwa msichana anayedaiwa pia ni changudoa zilidai kuwa, mwanamke huyo ni mke wa mtu na amekuwa akiingia ‘viwanja’ mumewe akiwa nje ya Jiji la Dar.
“Yule dada mbona ana mume wake, yaani kama ni kuumbuka ameumbuka. Jamaa yake huwa anasafiri na yeye hapo ndipo hupata muda wa kutoka,” kilisema chanzo hicho.
Imeandikwa na: Chande Abdallah, Denis Mtima, Nyemo Chilongani na Deogratius Mongela. 

0 comments:

Post a Comment