Stori: Richard Bukos na Makongoro Oging
MTOTO Grace Simon (14) aliyewahi kuripotiwa na gazeti hili kuwa anapata mateso kutokana na mwili wake kuzidi kufumuka kila kukicha, hatimaye amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Akizungumza kwa masikitiko mama wa mtoto huyo, Ashura Ally alisema baada ya kuhangaika sehemu mbalimbali zikiwemo hospitali za Wachina, kwenye huduma za maombezi na sehemu nyinginezo bila mafanikio, sasa mwanaye huyo amefikishwa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
“Awali mwanangu alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa na tatizo kwenye ini na homoni zimepoteza uwiano na kumfanya afumuke bila mpangilio,” alisema mama huyo.
Mama wa mtoto ameendelea kuomba msaada wa hali na mali ikiwemo ushauri unaoweza kuokoa afya ya mwanaye kupitia namba 0769319446 na 0719465443.
0 comments:
Post a Comment