Thursday, February 6, 2014


Na Gladness Mallya na Hamida Hassan
Unaamini kurogwa? Hebu msikie huyu! Baada ya kuugua kwa muda mrefu, msanii wa filamu za Kibongo ambaye alikuwa ni mama mlezi wa klabu ya waigizaji ya Bongo Movie Unity (Bongo Muvi), Herieth Chumila, amefunguka kuwa ametupiwa majini na wenzake katika tasnia hiyo.
Herieth Chumila anayedai kutupiwa jini.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Herieth alisema ni muda mrefu tangu alipoanza kuugua ambapo alikwenda hospitali mbalimbali, kwa mashehe na kutumia dawa za kienyeji zikiwemo za ‘ki-sunna’ lakini hakukuwa na mafanikio yoyote kwani hakugundulika kuwa na ugonjwa wowote.
Alisema kila alipokuwa akiombewa, majini yalikuwa yanasema yametokea Bongo Movie Unity na sababu za kutupiwa ni kwa kuwa eti alijiingiza kwenye kila kitu hivyo wakaamua kumkomesha.
Baada ya kushindikana kote huko, Herieth kwa sasa anashinda kanisani kwa Nabii Yasip Bendera wa Kanisa la Ufunuo huko Yombo-Buza, Dar, akiombewa na afya yake inaendelea vema.
“Kweli uchawi upo, hao Bongo Movie wamenitupia majini. Jamani nimeugua sana ila kwa sasa ninaendelea vizuri baada ya kuombewa. Namshuru sana Mungu kwa kunipa nafuu,” alisema Herieth kwa uchungu.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere hakupatikana kwa simu kujibu madai hayo.

0 comments:

Post a Comment