Friday, February 7, 2014


Doreen Ponera ‘Pipi’.
Na Gladness Mallya
MSEMO wa ‘Enendeni mkaijaze duni’ umekuwa na maana kubwa kwa msanii wa  muziki wa kizazi kipya Bongo, Doreen Ponera ‘Pipi’ ambapo amezidi kuongeza  familia kwa kujifungua mtoto wa pili wa kiume.
‘AKimng’ata sikio’ mwandishi wetu  mwanzoni mwa wiki hii, rafiki wa karibu na msanii huyo (jina tunalo) alisema Pipi alijifungua hivi karibuni katika Hospitali ya Misheni ya Herbert Kairuki, Mikocheni jijini Dar na kwamba mtoto huyo amempa jina la Brandon.
Baada ya kumwagiwa ‘upupu’ huo, gazeti hili lilimtafuta Pipi ili kuthibitisha madai hayo ambapo alisema:
“Ni kweli nimejifungua mtoto wa pili ambaye pia ni wa kiume, ninamshukuru Mungu kwani nimejifungua salama na kawaida tofauti na mwanzoni nilijifungua kwa operesheni, nina furaha sana kila ninapowaangalia wanangu siamini kama mimi ndiye niliyewazaa.”

0 comments:

Post a Comment